Nyuma ya Mapazia
By
Ben Mtobwa
Book Summary:
Tanzania iliingia katika uchaguzi mkuu ulioshirikisha vyama vingi
kwa mara ya kwanza mwaka wa 1995. Kampeni kubwa za kitaifa na kimataifa
zilifanyika hadharani na sirini. Yako mengi yaliyokuwa yakiendelea
‘Nyuma ya Mapazia’. Mengi ya kutisha na kuogofya, na ambayo yaliambatana
na matumizi makubwa ya pesa, mauaji ya kikatili na ujambazi usio na
kifani. Joram Kiango, Inspekta Kombora na kikosi kizima cha polisi
wanagonga mwamba katika harakati zao za kutatua kizungumkuti hicho.
Kutokweka kwa King Halfan King na maiti ya mpenziwe kupatikana ikielea
ufukweni wa Bahari ya Hindi kunazidisha maswali mengi bila majibu. Hata
hivyo, kizungumkuti hiki kitatatuliwa?